Multimedia Newsroom
Wednesday, 28 August 2013
Available in
  • ENG
  • SW

  • Tanzania: Maisha ya Hatari ya Watoto Wachimba Dhahabu

    Feature
    Duration : 4m 57s
    (Dar Es Salaam) – Watoto wenye umri mdogo wa hadi miaka minane wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu ya Tanzania, ikiwa na hatari kubwa kwa afya zao na hata maisha yao, shirika la Human Rights Watch imesema katika ripoti iliyotolewa leo. Serikali ya Tanzania inapaswa kukomesha ajira kwa watoto katika uchimbaji mdogo mdogo wa dhahabu, ikiwa ni pamoja na katika migodi isiyo rasmi, na isiyo na leseni, na Benki ya Dunia na nchi wahisani wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi.
    Ripoti yenye kurasa 96, “Kazi ya Sulubu yenye Sumu: Ajira kwa Watoto na Kujiweka Wazi kwa Zebaki katika Migodi Midogo Midogo ya Dhahabu ya Tanzania,”inaelezea jinsi gani maelfu ya watoto wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu yenye leseni na isiyo na leseni Tanzania, nchi ya nne kwa ukubwa kwa uzalishaji wa dhahabu barani Afrika. Wanachimba na kupekesha mashimo marefu , yasiyo imara, wakifanya kazi chini ya ardhi kwa kupeana zamu kwa hadi masaa 24, na kusafirisha na kutwanga mifuko mizito ya mawe ya dhahabu. Watoto hawa wanakuwa katika hatari ya kujeruhiwa kwa mashimo kuporomoka na ajari zinazoweza kutokana na vifaa wanavyotumia, vile vile matatizo ya kiafya ya muda mrefu kutokana na kujiweka wazi kwa zebaki, kuvuta vumbi, na kubeba mizigo mizito. Kijana mdogo wa miaka 17 aliyenusurika katika ajali ya shimo aliiambia shirika la Human Rights Watch, “Nilidhani nimekufa, niliogopa sana.”“Vijana wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta wamekwama katika mzunguko mbaya wa hatari na kukata tamaa,” alisema Janine Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch “Tanzania na wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni ao katika mafunzo ya ufundi stadi.”